Mchuano mkali wa ndondi kati ya Conor McGregor na mwanandondi Floyd Mayweather Jnr hatimaye umemalizika huko Las Vegas, Nevada nchini Marekani, baada ya kuchelewa kuanza kwa muda wa lisaa moja hivi. Floyd Mayweather Jnr ameibuka mshindi katika mchuano huo. Maelfu ya watu walifika katika mji wa Las Vegas katika jimbo la Nevada nchini Marekani , kutizama mchuano huo mkali wa ndondi, uliofanyika usiku wa kuamkia leo Jumapili. Masumbwi hayo yalikuwa ya raundi kumi. Awali wachanganuzi walisema kuwa Floyd Mayweather Jnr alikuwa ameanza kulemewa katika raundi tatu za mwanzo na mpinzani wake, kabla ya kujizoazoa na kuanza kumrushia makonde mazito mazito Conor McGregor, ambaye alionekana kulemewa hasa kuanzia raundi ya saba. Lakini Conor McGregor , Alishindwa kuhimili makonde mazito ya Maywheather na kushindwa kumaliza raundi ya 10. Mayweather , alipig...