Wilaya ya Same yatia mkazo maandalizi ya Tanzania ya viwanda kwa kulima pamba bora

Hayo ameyasema Mkuu wa Wilaya hiyo Mh: Rosemary Senyamle Staki alipokuwa Kata ya Kisiwani kwenye ziara aliyoongozana na Katibu Tawala Wilaya pamoja na Afisa Kilimo Wilaya. Wakiwa Kisiwani walipata nafasi ya kutembelea Shamba la Mkulima wa Pamba amaarufu kama Mzee Selemani Pesa 

DC alimpongeza Mkulima huyo kwa kulima zao hilo la Biashara kwa ubora wa juu wa pamba hiyo ambayo imechangia kuitangaza zaidi Wilaya ya Same katika nyanja ya Kilimo cha Pamba hapa nchini. Aidha Mkulima huyo aliuambia ugeni huo kuwa pamba aliyovuna Msimu huu imepata ubora na kufikia daraja la juu 2017 kwa zaidi ya 80% ya pamba iliyovunwa na kuuzwa kwa Tshs. 1200 kwa kilo moja.

DC huyo alisema ili Tanzania ya viwanda ifanikiwe vizuri ni muhimu kujiandaa na kuongeza kilimo cha mazao ya Biashara ili malighafi zipatikane hapa hapa Nchini kwa kiwango kikubwa zaidi ya tunachozalisha sasa.

IMG-20170829-WA0002.jpg
Hapa viongozi hao wa Wilaya wakiongea na Mkulima wa Pamba Wilayani humo Mzee Selemani Pesa.

Comments

Popular posts from this blog

Kumbukumbu ya kuundwa kwa chama cha AA mwaka 1927 chini ya Sesilia Matola

Dodoma: Dereva wa Tundu Lissu, Dr. Mashinji, Watakiwa kuripoti Polisi, Magari 8 Nissan Patrol yakamatwa

Jinsi ya kutengeneza SABUNI ya kipande