Sakata la IMMMA: Rais wa TLS, Tundu Lissu atoa maazimio ya Baraza la Uongozi. Wapanga kugoma siku mbili
Baraza la uongozi la TLS lilifanya kikao jana tarehe 26/08/2017 kujadili shambulio la mabomu. Baraza limepata taarifa kikundi cha watu kadhaa kikiwa kimevalia sare za jeshi la polisi na wakiwa na silaha za moto kiliwateka nyara walinzi binafsi wa Immma advocates na kuingia ndani na kutega milipuko na madumu manne ya mafuta ya petroli katika jengo zilizopo ofisi hizo.
Muda mfupi baadae, milipuko hio ililupuka na kusababisha uharibifu katika jengo hilo na majengo jirani, kwa sababu ilikuwa usiku, hakuna mtu yeyote alieumia au kupoteza maisha kutokana na shambulio hilo.
Baraza la uongozi linatoa taarifa ifuatayo kutokana na shambulio hilo dhidi ya Immma advocates.
- Baraza limeshtushwa na kuhuzunishwa na kuvamiwa ofisi za Immma Advocates.
- Pamoja na kuwa ni mapema kufahamu mhusika na sababu zake, baraza linalaani uvamizi kwani unahatarisha uhuru wa sheria na mahakama.
- Kitendo cha kushambuliwa kilikuwa na lengo la kuzuia utekelezaji wa wanasheria hao.
- Kilikuwa na lengo la kuwatisha mawakili hao na wameomba niwaambie kuwa hawatotishishika.
- Kitendo hicho kinakiuka sheria za nchi na mikataba ya kimataifa ambayo nchi yetu imeingia.
Waandishi wa habari, nasema yote kwa sababu ni muhimu tukafahamu tukafahamu kazi walizokuwa wanazifanya ambazo zinaweza kuwa sababu.
- Immma wanawakilisha wateja mbalimbali, wanakilisha kampuni ya madini ya Acacia ambayo ina mgogoro mkubwa na serikali
- Inamuwakilisha katibu mkuu wa CUF
- Ni sehemu ya mawakili inayomuwakilisha anaeongea nanyi.
- Wakili wa Imma amefungua kesi dhidi ya askari aliemdhalilisha mahakamani.
Baraza la uongozi la TLS
- Linavitaka vyombo vya ulinzi na usalama kuchunguza haraka tukio na kupatikana kwa wahusika.
- Kuwahakishia ulinzi wa kutosha mawakili wa Imma kulingana na vitisho wanvyopata, ni wajibu wa kisheria wa serikali.
- Linawataka wanachama wote wa TLS nchi nzima kususia kuhudhuria kwa siku mbili za Jummanne na Jumatano mahakamani na kwenye mabaraza kuwaunga mkono walioshambuliwa kwa mabomu. Shambulio dhidi ya wakili mmoja linatakiwa kuwa shambulio dhidi ya mawakili wote, Immma hawatoweza kwenda mahakamani kwa siku kadhaa kwa sababu vitendea kazi vyao vimeharibiwa.
- Baraza linafanya utaratibu wa haraka kuonana na uongozi wa juu wa jeshi la polisi na usalama wa taifa kujadili kuvamiwa kwa mawakili, wawasaidie kujua nani anaewashambulia
- Linawataka wananchi kuhakikisha linalinda usalama wa mawakili ili waweze kutekeleza wajibu wao, wakitishwa watashindwa kutimiza wajibu wao wa kuwawakilisha mahakamani, tunawaomba watanzania mpaze sauti zenu.
Comments
Post a Comment