Fahamu utajiri uliopo kwenye uwekezaji wa dhamana za Serikali(Treasury Bills & Bonds)

UTAJIRI MKUBWA ULIOPO KWENYE UWEKEZAJI WA DHAMANA ZA SERIKALI

Uwekezaji kwenye dhamana za serikali umegawanyika makundi mawili.

i) Dhamana za muda mfupi (treasury bills)
ii) Dhamana za muda mrefu (treasury bonds)

Kwa nchi yetu ya Tanzania biashara ya dhamana za serikali inasimamiwa na Benki Kuu ya Tanzania (BOT) kwa niaba ya serikali ya Tanzania.

Dhamana za muda mfupi (treasury bills)
Hizi ni dhamana za muda mfupi ikimaanisha zinaiva ndani ya mwaka mmoja. Lengo kubwa hasa kwa serikali kuweka Treasury bills ni kupata fedha kwa ajili kukabiliana na mapungufu ya fedha katika bajeti na pale inapohitaji fedha kwa haraka.

Dhamana za muda mfupi zipo katika makundi manne kutegemea na mda zitakapoiva: ya siku 35, siku 91, siku 182 na siku 364.

Uwekezaji katika Treasury bill una faida zifuatazo kwa mwekezaji;
i)Hazina hatari yoyote kubwa (risk free) kwa mwekezaji na ni uwekezaji wa uhakika kwa sababu zinatolewa na serikali.

ii)Zaweza kuhamishika kutoka umiliki wa mtu mmoja kwenda kwa mwingine. Ikimaanisha pale mwekezaji anapotaka kuuza anaweza akafanya hivo.

iii)Zaweza kutumika kama dhamana za kuombea mikopo kwenye taasisi za fedha bila usumbufu wowote kwa sababu thamani ya treasury bill coupon haibadiliki kwa hiyo ni rahisi kwa taasisi za fedha kuzipa kipaumbele kutumika kwenye dhamana.

iv)Gawio ni kubwa pale unapowekeza kwenye treasury bills zaidi hata ya kuwekeza kwenye taasis yeyote ya fedha kupitia fixed deposits. (namaana ya kwamba riba katika treasury bills ni kubwa maradufu ya riba za benki)

Soko la treasury bills
Biashara na soko la treasury bills zinafanyika kwa njia mbili;

a) Soko la awali (primary market) hapa ni pale banki kuu ya Tanzania inapotoa kwa mara ya kwanza treasury bills kwa wawekezaji.

b) Soko la pili (secondary market) hii inahusisha kuuza na kununua treasury bills na hii inafanyika Dar es salaam stock exchange DSE. Hapa ndipo pale mtu anapotaka kuuza treasury bills anayoimiliki anaweza kwenda kuuza.

Kianzio cha kuwa mwekezaji wa moja kwa moja kwenye treasury bills kwa Tanzania ni sh. 5,000,000. Ina maana kwamba ukiwa na mtaji wa kuanzia milioni tano basi unaruhusiwa moja kwa moja kushiriki kwenye mnada wa treasury bills (treasury bills auction).

Kwa wawekezaji wa mtaji chini ya milioni tano basi wao watashiriki kwenye mnada kupitia primary dealers ambao kwa urahisi ni mabrokers na commercial banks

Primary dealers ambao wamethibitishwa na BOT ni hawa wafuatao (ambao wale wenye mitaji chini ya milioni tano watapitia kwao) Akiba Commercial Bank Ltd, Citibank (T) Ltd, CRDB Bank Ltd, Diamond Trust Bank (T) Ltd, Eurafrican Bank (T) Ltd.Exim Bank (T) Ltd. Habib African Bank Ltd. International Commercial Bank (T) Ltd. Kenya Commercial Bank (T) Ltd.NBC Limited. NMB Ltd. Stanbic Bank (T) Limited Standard Chartered Bank Ltd.Orbit Securities Co. Ltd. Rasilimali Limited Solomoni Securities Ltd. Core securities Ltd. Tanzania securities Ltd. Vertex International Securities.

Unapata vipi pesa kupitia dhamana za muda mfupi?
Serikali kupitia BOT inapotoa treasury bills zinakuwa katika mfumo wa zabuni ikimaanisha kwamba wawekezaji watatakiwa kwa mfano kusema watanunua kila shilingi 100 ya serikali kwa kiasi gani? (hatua hiyo ya kwanza inaitwa bidding)

Ili kupata faida kwa wawekezaji wanatakiwa kutoa bei ambayo ipo katika discout, ikiwa na maana mwekezaji anaweza kununua shilingi 100 ya serikali kwa shilingi 93 hivo mda wa kuiva ukifika atapata faida ya shilingi 7.

Mfano serikali imetoa treasury bills ya siku 365. Kisha mwekezaji akaweka bid ya kununua kila shilingi 100 kwa shilingi 75. Kama mwekezaji atafanikiwa kwenye zabuni hiyo atapata treasury bill yenye (face value) ya Tzs 100,000,000 ingawaje kiasi alichotoa ni Tzs 75,000,000 kwa sababu ndicho kiasi alicho bid katika kabrasha la zabuni yake.

Baada ya treasury bills kuiva yaani kutimia siku 365, mwekezaji atalipwa na BOT kiasi cha TZS 100,000,000 ambayo italeta faida ya (TZS 100,000,000-TZS 75,000,000= TZS 25,000,000). Hivo faida itakuwa ni TZS 25,000,000.

Ukiweka katika asilimia ni kama ifuatavyo; 
- Kanuni ya kukokotoa riba katika treasury bills:
Riba=(F-P)/P ×(365×100)/N

F= face value ya treasury bills ambayo ni 100
P= bidding price ambayo ni 75 kama mfano unavosema
N= idadi ya siku treasury bills itapoiva mfano wetu ni siku 365

Riba= (100-75)/75 ×(365×100)/365
=0.3333×100
Riba = 33.33%

Ikiwa na maana kwa pesa ambayo utatoa kununua treasusry bills utapata gawio la asilimia 33.33% ndani ya siku 365 yaani mwaka mmoja tu.

Piga mahesabu kama umewekeza milioni 100 ambazo huna matumizi nazo ina maana baada ya siku 365 utakuwa na faida ya kama milioni 30 ambazo hata kujazitolea jasho.

Nataka pia kuwamegea siri kwamba mabenki ya kibiashara na wafanyabiashara wakubwa ndio wamekuwa wakitajirikia hapa kwani wao wanawekeza kuanzia bilioni na kwenda juu. Kwa hiyo unaweza kufikiri ni pesa kiasi gani wanatengeneza.
Kuna watanzania wengi sana wana mamilioni ya pension benki hizi ndizo fursa za kuchangamkia ambazo huwezi kuzisikia zikitangazwa kwa maana ndipo pesa ilipo.

Kama hujaelewa waweza acha comment yako hapa then ntakujibu..

Comments

Popular posts from this blog

Kumbukumbu ya kuundwa kwa chama cha AA mwaka 1927 chini ya Sesilia Matola

Dodoma: Dereva wa Tundu Lissu, Dr. Mashinji, Watakiwa kuripoti Polisi, Magari 8 Nissan Patrol yakamatwa

Jinsi ya kutengeneza SABUNI ya kipande