Waziri wa zamani, William Ngeleja aitwa na kuhojiwa na Ofisi ya Mkurugenzi wa Makosa ya Jinai (DCI)

Mbunge wa Sengerema, William Ngeleja amehojiwa kwa saa moja katika Ofisi ya Mkurugenzi wa Makosa ya Jinai (DCI), jijini Dar es Salaam leo Jumatatu Septemba 11.

pic+ngelej.jpg

Ngeleja ambaye pia amewahi kuwa Waziri wa Nishati na Madini wa awamu ya nne, aliwasili katika ofisi hiyo saa nne asubuhi akiwa peke yake ambapo alikutana na DCI saa tano na kuondoka saa sita na nusu mchana bila kusema alichohojiwa.

Hatua ya Ngeleja kufika ofisini hapo ni kuitikia wito wa Mkuu wa Jeshi La Polisi (IGP), Simon Sirro ambaye aliwataka watuhumiwa waliotajwa katika ripoti ya Tanzanite na Almasi kuripoti kwenye ofisi hiyo kwa ajili ya mahojiano wakati uchunguzi ukiendelea


Chanzo: Mtanzania

Comments

Popular posts from this blog

Jinsi ya kutengeneza SABUNI ya kipande

Kumbukumbu ya kuundwa kwa chama cha AA mwaka 1927 chini ya Sesilia Matola