Siku ya 7: Tundu Lissu bado amelazwa ICU na hawezi kula, kuamka na kuzungumza na yeyote
Imeelezwa Mwanasheria Mkuu wa Chadema , Rais wa TLS na Mbunge wa Jimbo la Singida mashariki Mhe Tundu Lissu kwa siku saba sasa bado amelazwa ICU na hawezi kula, kuamka na kuzungumza na yeyote zaidi ya madaktari.
Tundu Lissu anaendelea kupokea matibabu katika hospitali ya Nairobi nchini Kenya, baada ya kupigwa risasi na watu wasiojulikana mjini Dodoma wiki iliyopita.
My take: Tuendelee kumwombea Mh. Tundu Lissu katika kipindi hiki kigumu anachopitia. MUNGU amlinde, akamponye na kumfanyia wepesi katika uhitaji wake
==========UPDATES

MBOWE ATETA JUU YA HALI YA MH.LISSU
Mwenyekiti wa Chadema, Freeman Mbowe amesema kuwa hivi sasa Mbunge wa Singida Mashariki, Tundu Lissu anaweza kuongea na kula kidogo.
Akizungumza na waandishi leo Alhamisi jijini Nairobi, Mbowe amesema taarifa za kwamba Lissu amepata maambukizi katika kifua ambayo yanatishia maisha yake siyo za ukweli.
Mbowe amesema hali ya Lissu inabadilika kila siku hivyo amewahakikishia wananchi kuwa anaendelea kurejea katika hali yake.
Amesema Lissu ameweza kuonana na baadhi ya waliomtembelea kwa maelekezo ya madaktari ambao wanamtibu.
"Pamoja na kwamba kuna watu wengi wanataka kumuona lakini ni wachache wanaoruhusiwa kumuona kwa kuwa madaktari wanataka apumzike,"amesema Mbowe.

Comments
Post a Comment