NYARAKA: Wizara ya Madini iliidhinisha thamani ya Almasi ya Sh. Bilioni 14 kama thamani ya awali kusubiri mnada Ubelgiji

Naona sasa kumekucha

Taarifa zinaonyesha kwamba thamani ya Madini ya almasi iliyokamatwa uwanja wa ndege ilikuwa ni thamani ya awali. Ni wazi kwamba almasi huuzwa kwa mnada huko Ubelgiji na bei ya mnada huangalia mnada umeendaje,inaweza kupanda au kushuka,lakini muuzaji huweka bei ya awali

Nyaraka hii inaonyesha wizara ya nishati na Madini ikikiri kwamba thamani ya Madini hayo ni ya awali tu(PROVISIONAL) na kwamba thamani halisi ingejulikana siku ya mnada wa Madini Belgium
document 3.PNG 
Hii ina maana gani? Ng'ombe alikuwa anapelekwa mnadani akapangiwe bei, ila nyumbani kama familia timekadiria kwamba pengine anaweza kuwa wa bei fulani, tunampa muuzaji aende na kadirio la chini sana,lakini apambane afikie thamani ya juu sana

Kwa hiyo kusema kwamba mwadui walidanganya,tulitaka mwadui wageuke watabiri wajue nani atanunua kwa shilingi ngapi?
document 2.PNG 
Je tunajua maana ya PROVISIONAL?

Wizara inakiri kwamba ni kilo 19! Sasa inamlaumu nani?

Kuhusu mrabaha,huu nao alikuwa wa awali,na ulipigiwa hesabu kutokana na thamani ya awali ya Madini kabla hayajafikishwa mnadani,kwa nini nasema ni mrabaha wa awali? Nani anajua kwamba huko mnadani tungeuza almasi hiyo kwa hata bilioni mia? Au bilioni ishirini? Au tusiuze kabisa? Kwa hiyo mwadui pia walilipa PROVISIONAL Royalty,kama mnada ungekuwa mtamu,mwadui hawanaga hiyana,wangejazia Royalty hata kama ingekuwa ya bilioni 700,lakini kwanza je mnada ungetoa bei nzuri?

document 4.PNG 
Lakini pia kamishna wa Madini aliidhinisha Almas hiyo isafirishwe kwenda nje,bila shaka kamishna wa Madini ni mtu mtaalamu aliyeiva anayejua ABC za biashara ya almasi na anaelewa nini maana ya PROVISIONAL
document 1.PNG

Sasa tuweke Court Room Drama

Umesema umetaifisha Almasi kwa sababu Mwadui walitangaza thamani pungufu:

Serikali: ndio

Soma hii karatasi:
Serikali: nimesoma

Imeandikwa na nani?

Serikali:imeandikwa na serikali ya jamhuri ya muungano kupitia wizara ya nishati na Madini

Unaelewa maana ya provisional value?

Serikali; ndio,ni thamani ya awali

Kwa hiyo thamani halisi ingejulikana kwenye mnada?

Serikali: ndio

Kwa hiyo uliposema hawakutaja thamani halisi,hawa mwadui wangejuaje thamani halisi kabla ya mnada?

Serikali:kimya

Kamishna wa Madini alitoa kibali cha kusafirisha?

Serikali:ndio

Kwa hiyo taratibu zote zilifatwa?

Serikali: ndio

Kwa nini ulitaifisha kama unajua thamani halisi ingejulikana Belgium na taratibu zote zilifatwa

Serikali: kimya

Comments

Popular posts from this blog

Jinsi ya kutengeneza SABUNI ya kipande

Kumbukumbu ya kuundwa kwa chama cha AA mwaka 1927 chini ya Sesilia Matola