Arusha: Mtekaji wa watoto afariki dunia kwa kupigwa risasi wakati akijaribu kutoroka
Mtuhumiwa Samson Petro ambaye ndie mtekaji na muuji wa watoto wawili Maureen na Ikram amefariki dunia kwa kupigwa na risasi wakati akitaka kutoroka mikononi mwa Polisi jijini Arusha.
Mtuhumiwa alipigwa risasi mbili za miguu wakati akijaribu kutoroka na ndipo alipofariki dunia akiwa hospital ya Mount Meru.
Hapo awali Usiku wa tarehe 2 Septemba kijana mwenye umri wa miaka 18, Samson Petro alishikiliwa na polisi kwa tuhuma za kuteka watoto katika mkoa wa Arusha na Geita.
Kamanda wa Polisi mkoani Geita, Mponjoli Mwabulambo alithibitisha taarifa hizo za kukamatwa kwa mtekaji huyo.
Mwabulambo alisema kuwa kijana huyo alikamatwa katika nyumba ya kulala wageni ya Shitungului iliyopo mji mdogo wa Katoro akiwa na mtoto mdogo nmwenye miaka miwili.
Alisema mtuhumiwa alimficha mtoto huyo katika chumba namba 11 cha kulala wageni iitwayo Shitungulu wakati akisubiri mpango wake wa kutaka alipwe shilingi milioni nne na wazazi wa mtoto huyo Omben Mshana na Elizabeth Ombeni.
Habari zaidi soma;.
Kukithiri kwa vitendo vya Utekaji wa watoto/kidnapping katika Jiji la Arusha
ARUSHA: Watoto wawili kati ya wanne waliokuwa wametekwa wapatikana wakiwa wamekufa
Askari wa FFU akamatwa sakata la utekaji watoto
GEITA: Mtekaji wa watoto Arusha, Geita anaswa na Polisi
Mtekaji akiri kuua watoto 2, kuwatumbukiza shimoni
Comments
Post a Comment