Waziri Charles Mwijage amuomba rais Magufuli radhi kwa kumkwaza, aahidi kufanyia kazi maelekezo yake


Waziri wa viwanda biashara na uwekezaji ndugu Charles Mwijage amemuomba rais Magufuli msamaha kwa kumkwaza katika kazi na kuahidi kufanyia kazi maelekezo yake.

Aidha katika hatua nyingine waziri Mwijage amemuomba rais Magufuli kutomkumbusha tena majukumu yake kwakuwa kwa kufanya hivyo atakuwa anamuumiza kisaikolojia.

Mapema leo Rais Magufuli ametamka waziwazi kuwa ndugu Charles Mwijage ni miongoni mwa mawaziri wanaomkwaza kiutendaji na kuenda mbali zaidi kwa kuwaita baadhi ya mawaziri wake kuwa ni wapumbavu.

#PambaneniNaHaliYenu

Si muondoke humo mumuachie? Yanini kung'ang'ania na masimango yote hayo?

Comments

Popular posts from this blog

Jinsi ya kutengeneza SABUNI ya kipande

Kumbukumbu ya kuundwa kwa chama cha AA mwaka 1927 chini ya Sesilia Matola