Serikali itazingatia? Mambo muhimu ya kuboresha kwenye Ofisi za Umma

Taasisi ya Misa Tanzania imetoa ripoti maalum inayoonyesha hali halisi ilivyo juu ya upatikanaji wa taarifa kutoka katika ofisi nyingi za umma kupitia utafiti uliofanywa kwenye Mikoa 7 mikubwa nchini ambayo ni Kigoma, Dar, Mwanza, Mbeya, Arusha na Dodoma na Mtwara.

Ripoti hiyo inaeleza kuwa, Katika ofisi za umma hasa Halmashauri za Jiji, kumekuwa na mkwamo mkubwa sana wa kupatikana kwa taarifa muhimu ambako kunachangiwa na changamoto za uduni wa teknolojia, uzamani, elimu na maslahi binafsi ya watumishi wa umma.

Changamoto hizo kwa muda mrefu sasa zimekuwa zikiwanyima wananchi haki ya msingi ya kupata taarifa na kujua mambo muhimu yanayowahusu.

Kwa kuliona hilo, MISA wakaja na mapendekezo haya ili serikali ichukue hatua;

1. Kwa kuwa tayari kuna sheria (Information Act - 2016), Serikali iitilie mkazo ili watumishi wote wa umma waijue vyema na waanze kuifanyia kazi.

2. Kuwe na semina maalum, warsha na makongamano kwa watumishi wa umma juu ya uhuru wa habari na umuhimu wa wananchi kupata taarifa zitakazofaa kwa ajili ya maendeleo.

3. Kuanzishwe madawati maalum katika ofisi za serikali ambayo yatarahisisha utoaji wa taarifa kwa wananchi. (mfano mtu anaweza kwenda kwenye hivyo vituo/madawati na kuchukua vipeperushi vyenye taarifa anazozitaka na kuondoka zake).

4. Kuwe na namna ambayo wananchi wataweza kusimamia zoezi zima la upatikanaji wa taarifa ktk ofisi za umma au hata zile binafsi ambazo zinaendeshwa kwa fedha za wananchi.

5. Serikali iweke msisitizo kwa ofisi za umma kutumia TEHAMA na teknolojia za kisasa kwa ujumla katika utoaji wa taarifa kulingana na sera inavyoelekeza. Ni aibu mpaka karne hii bado kuna taasisi zinashindwa kujibu barua pepe kwa wakati.

6. Zipo baadhi ya ofisi zinatumia mifumo ya kisasa lakini nyingi bado ni za kizamani na hazina hata kompyuta. Serikali ijitihadi kuongeza idadi ya vitendea kazi vya kisasa.

7. Kuna umuhimu wa kuhamia kwenye mfumo wa kisasa katika kutunza mafaili. Ni aibu unatumiwa barua na ndani ya wiki moja inakuwa ngumu kuipata. Vipi ikiwa mwaka?

Comments

Popular posts from this blog

Jinsi ya kutengeneza SABUNI ya kipande

Kumbukumbu ya kuundwa kwa chama cha AA mwaka 1927 chini ya Sesilia Matola