PICHA 2:Wafanyabiashara Na Serikali Bado Utata Katika Ujenzi Mpya Wa Soko La “SIDO” Mbeya

TAREHE-18/08/2018

Kutoka Mkoani Mbeya leo hii Katibu tawala amegomewa kuongea na wafanyabiashara wa soko lililoungua la SIDO mara baada ya wananchi hao kuanza kushusha matofari ya ujenzi wa vibanda vyao vilivyo ungua ilihali serikali imepiga marufuku kuendelea na shughuli za ujenzi wa vibanda hivyo hadi pale uchunguzi utakopo kamilika tarehe 23 Agost 2017.
Wafanyabiashara hao pamoja na mwenyekiti wa soko hilo la SIDO Ndugu Charles Syongawamekinzana juu ya uamuzi wa serikali wa kusimamisha ujenzi wa soko hili hadi ifikapotarehe 23 wakidai kwamba hali ngumu kwao kwani wengine ni wadaiwa na taasisi za kifedha hivyo wanatakiwa kuanza biashara mapema ili kuweza kukamilisha urejeshaji wa fedha hizo walizokuwa wamekopa ili kuendesha biashara zao.
Hata hivyo kutokana na kuto kuwa na maelewano baina ya wafanyabiashara hao kuanza kuleta mgomo imepelekea jeshi la polisi kuanza kulipua mabomu ya machozi ili kuwatawanya wafanyabiashara hao ili kupisha shughuli nzima za uchunguzi hadi pale utakapo kamilika ndipo wataendelea na shughuli za ujenzi wa soko hilo.
.
Maduka yaliendelea kufungwa huduma muhimu kwa mahitaji ya wakazi wa Jiji la Mbeya ziliendelea kusimama kwa siku ya pili mfululizo.

Comments

Popular posts from this blog

Jinsi ya kutengeneza SABUNI ya kipande

Kumbukumbu ya kuundwa kwa chama cha AA mwaka 1927 chini ya Sesilia Matola