- Get link
- X
- Other Apps
Mbunge wa Mbozi “Pascal Haonga” Azidi Kusota Rumande Hadi Uchunguzi Utakapo Kamilika
Kamanda Nyange amesema sababu za kumtia mbaroni Haonga ni kutokana na kufanya mkutano bila kibali cha polisi katika mji mdogo wa Mlowo-Mbozi na kuwahamasisha wamiliki wa malori na abiria kuandamana kwenda ofisi ya Mkuu wa Mkoa huo, Chiku Galawa.
Amesema Haonga alifanya mkutano huo jana Jumatano, Agosti 2 na alihamasisha madereva wa malori, wamiliki na abiria waende kumuona mkuu wa mkoa.
“Bado hatujakamilisha upelelezi na tutakapokamilisha muda wowote tutamfikisha mahakamani na kuhusu dhamana tutafikiria kumpatia dhamana ama laa,” amesema Kamanda Nyange.
Amesema lengo la mbunge huyo kuwataka watu hao wamuone mkuu wa mkoa ni kueleza kero yao juu ya adha ya usafiri baada polisi kupitia kitengo cha usalama barabarani kupiga marufuku malori kubeba abiria kutoka katikati ya mji wa Mlowo kwenda maeneo tofauti ya vijijini ambako hakuna usafiri mbadala zaidi ya malori.
- Get link
- X
- Other Apps
Comments
Post a Comment