EXCLUSIVE UPDATES: Uchaguzi Mkuu Kenya Agosti 8, 2017
OFFICIAL PRESIDENTIAL RESULTS:
01:20am August 09, 2017 UPDATE:
Tume ya Uchaguzi(IEBC) Imetangaza matokeo ya vituo 29,209 kati ya 40,883. Uhuru Kenyatta kura 6,044,745 (55.27%) na Raila Odinga kura 4,805,159 (43.93%).
09:00am August 09, 2017 UPDATE:
Tume ya Uchaguzi(IEBC) imetangaza matokeo ya vituo 36,912 kati ya 40,883. Uhuru Kenyatta kura 7,511,454 (54.62%) na Raila Odinga kura 6,124,426 (44.53%)
12:00pm August 09, 2017 UPDATE:
Tume ya Uchaguzi(IEBC) imetangaza matokeo ya vituo 38,341 kati ya 40,883. Uhuru Kenyatta kura 7,776,101 (54.4%) na Raila Odinga kura 6,394,921 (44.74%)
3:00pm August 09, 2017 UPDATE:
Tume ya Uchaguzi(IEBC) imetangaza matokeo ya vituo 39091 kati ya 40,883. Uhuru Kenyatta kura 7,915,044 (54.35%) na Raila Odinga kura 6,520,918 (44.78%)
August 10, 2017 - 06:30am UPDATE:
Uhuru - 8,030,150 (54.27%)
Raila - 6,634,331 (44.84%)
Valid votes: 14,795,377
Reporting Stations: 39,755 out of 40,883
live feed
![[IMG]](https://lh3.googleusercontent.com/blogger_img_proxy/AEn0k_uwbaT_V2MXiQE7ctXiM3Gz-nN5yjSPmnh6h9kxUPz7cNxbtNvuHsNhPnQXcm3P2NCh_bMQVBzmdfodR5VlMBVKV8pLCoCvPCdwSsOA61sDdj553Lq-6-3i3jbKnmYF2eje7uknjKpvJmy1CzPnHeMq=s0-d)
FACT 1: Kenya spent 49.9billion Kshs to organize this election and it's the most expensive since country's independence
KENYA: Uchaguzi Mkuu unafanyika leo, Wapiga kura milioni 19 watachagua Rais, Wabunge, Maseneta, Magavana, Madiwani na Wawakilishi wa Wanawake.
Raia wa Kenya wataamua nani atakuwa Rais wao na Makamu wa Rais kwa miaka 5 ijayo.
Ushindani mkubwa sana uko kati ya vyama vya Jubilee na NASA na wagombea wake wa Urais, Uhuru Kenyatta na Raila Odinga.
Pamoja na kura ya urais pia watapiga kura ya kuchagua magavana wa Kaunti, wawakilishi wa kata(madiwani) na wawakilishi wa Seneti na Bunge.
Fuatilia hapa kupata updates za uchaguzi huu unaohusisha takribani wapiga kura milioni 20 waliojiandikisha.
Waliojiandikisha: Milioni 19
Vituo vya kupigia kura: 40,000
Idadi ya Wakenya: Milioni 48
WASIFU WA WAGOMBEA KWA UFUPI
Tume Huru ya Uchaguzi Kenya (IEBC) iliwaidhinisha wanasiasa wanane ambao watawania urais katika uchaguzi mkuu huu wa Agosti mwaka huu.
Walioidhinishwa ni pamoja na Rais Uhuru Kenyatta wa chama cha Jubilee ambaye atakuwa anawania kuongoza nchi hiyo kwa muhula wa pili, na kiongozi wa muda mrefu wa upinzani Bw Raila Odinga ambaye anawania urais kwa mara ya nne.
Bw Odinga, aliyehudumu kama waziri mkuu katika serikali ya muungano ya Rais Mwai Kibaki kati ya 2008 na 2013, anawania urais chini ya umoja wa vyama vya upinzani kwa jina National Super Alliance (NASA).
Katika uchaguzi huu wa tarehe 8 Agosti, kutakuwa na wagombea wanne pia ambao ni wagombea huru (hawana vyama).
Abduba Dida
Anawania urais kupitia chama cha Alliance for Real Change (ARK) na muungano wa Tunza Coalition.
Alikuwa mwalimu wa shule ya upili ya Lenana jijini Nairobi.
Hii ni mara yake ya pili kuwania urais baada ya mwaka 2013 ambapo alipata kura 52,848 na kumaliza wa tano.
Cyrus Jirongo
Ni mwanasiasa na mfanyabiashara ambaye ni mara yake ya kwanza kuwania urais. Anawania kupitia chama cha United Democratic Party (UDP).
Alipata umaarufu kisiasa mwaka 1992 alipokuwa katika kundi la vijana wa chama cha KANU, Youth for KANU 1992 waliokuwa wakimfanyia kampeni Rais Daniel arap Moi wakati wa uchaguzi wa kwanza wa vyama vingi mwaka huo.
Ekuru Aukot
Anawania urais kupitia chama cha Thirdway Alliance Kenya (TAK), na ni mara yake ya kwanza kuwania urais. Alihudumu kama katibu katika Kamati ya Wataalamu waliosaidia kutunga Katiba Mpya ya Kenya ambayo iliidhinishwa na kuanza kutekelezwa mwaka 2010. Asili yake ni Kapedo, Turkana kaskazini magharibi mwa Kenya na amejitangaza kama mtu anayeleta mwamko mpya katika uongozi nchini Kenya. Amekuwa pia akitetea makabila madogo.
Japhet Kaluyu
Ni mgombea huru ambaye amerejea nchini Kenya hivi majuzi kutoka Marekani. Amejieleza kama mwalimu, mshauri na mwandishi ambaye ana uzoefu wa kufanya kazi Wall Street. Anasema amebobea katika utafiti katika sekta ya afya na msomi. Ni mara yake ya kwanza kuwania urais.
Joseph Nyagah
Ni mwanasiasa wa muda mrefu nchini Kenya ambaye alihudumu kama waziri wa vyama vya ushirika chini ya Rais Mwai Kibaki, na baadaye akawa mshauri wa Rais Kenyatta. Babake, Jeremiah Nyagah, alikuwa waziri wakati wa utawala wa mwanzilishi wa taifa la Kenya Jomo Kenyatta.
Bw Nyagah, ambaye alikuwahi kuwakilisha Kenya katika Umoja wa Ulaya, alihudumu kama mbunge wa eneo la Gachoka, Kaunti ya Embu mashariki mwa Kenya kabla ya kuteuliwa waziri. Anasema ndiye pekee anayeweza kutatua matatizo yanayoikumba Kenya, kutokana na uzoefu wake katika uongozi.
Akihojiwa na runinga ya NTV baada ya kuidhinishwa, alidokeza kwamba aliacha kazi yake ya kuwa mshauri wa rais baada ya kugundua kwamba ushauri aliokuwa anaoutoa haukuwa unafuatwa.
Prof Michael Wainaina
Yeye ni mgombea huru ambaye amekuwa mhadhiri wa fasihi katika Chuo Kikuu cha Kenyatta. Amekuwa mkosoaji mkuu wa mfumo wa sasa wa kisiasa Kenya na pia mchanganuzi wa siasa. Anasema aliamua kuwa mgombea huru kwa sababu vyama haviwapi nafasi vijana na wanawake.
Raila Odinga
Ni kiongozi wa chama cha Orange Democratic Movement (ODM) ambaye anawania chini ya muungano wa vyama vya upinzani kwa jina National Super Alliance (NASA). Aliwahi kuhudumu kama waziri mkuu wa kwanza wa Kenya, wadhifa ulioundwa kufuatia Mkataba wa Kitaifa ulioafikiwa kumaliza ghasia za baada ya uchaguzi mwaka 2007-2008, ambapo aligawana mamlaka na Rais Mwai Kibaki.
Ni mara yake ya nne kuwania urais Kenya. Mwaka 2013, akiwa bado na mgombea wake wa sasa Makamu wa Rais wa zamani Kalonzo Musyoka, alishindwa na Rais Uhuru Kenyatta. Alipinga matokeo hayo mahakamani lakini mahakama ikatupilia mbali kesi hiyo.
Uhuru Kenyatta
Anawania kwa muhula wa pili kupitia chama cha Jubilee Party ambacho asili yake ni muungano wa Jubilee wa vyama vya TNA na URP alioutumia kushinda urais mwaka 2013. Rais Uhuru Kenyatta wa Kenya ni mwanawe mwanzilishi wa taifa la Kenya Mzee Jomo Kenyatta. Mgombea wake mwenza ni Bw William Ruto kutoka eneo la Bonde la Ufa la Kenya. Wawili hao wanawaomba wapiga kura kuwachagua tena kuendeleza maendeleo ambayo wanaamini serikali yao imetekeleza katika kipindi cha miaka minne ambayo wamekuwa madarakani.
Bw Kenyatta aliwania urais mara ya kwanza 2002 dhidi ya Mwai Kibaki kupitia chama kilichokuwa kinatawala wakati huo, chama cha KANU cha Rais Moi aliyekuwa anaondoka madarakani baada ya kuongoza kwa miaka 24. Alishindwa na akawa kiongozi wa upinzani na kwa pamoja na Bw Odinga wakafaulu kupinga Katiba Mpya iliyopendekezwa mwaka 2005. Mwaka 2007, alimuunga mkono Rais Kibaki uchaguzini.
========
UPDATES:

Vijana wa Kaunti ya Kisumu wakiwa kwenye mstari wakisubiri kupiga kura.
Kaunti ya Siaya nao hawajataka kuwa nyuma.
![[IMG]](https://lh3.googleusercontent.com/blogger_img_proxy/AEn0k_t_jxeL9b-Mf8K_7AGVqaEoER4eEJzqG1N5eGjrhI3wiy910De5mcaRxqWTx6XL6kl-gRtSYlUnOGHIajFY05Vt9anrlHyh2DolapeYdHNSxrsbwJLPhy9rlmzGa2kOtYibc0kPqelky5KjmCM3mnuNAw=s0-d)
Man on a life support machine casts his vote at Dandora Primary School
LIVE TEXT FEED:
08:50am updates
> Rais Uhuru Kenyatta amewataka wakenya wajitokeze kwa wingi kuchagua viongozi wanaowapenda
> NASA wameamua kufuta kauli yao dhidi ya KDF baada ya kuhakikishiwa kuwa kila kitu kitaenda kwa mujibu wa taratibu na sheria
> Waangalizi wa EU wameridhika na mwenendo unaoonekana hadi sasa
> Wakenya wengi wamekiri kuwepo kwa propaganda kwa njia ya mitandao ya kijamii na hivyo kuwachanganya wengi
09:50am updates
![[IMG]](https://lh3.googleusercontent.com/blogger_img_proxy/AEn0k_tedyyuOOuNA10rpswba1PZHt2IRSXddD5Gu2LgSS0ot0uvs5kUeRz2tNL2DV_u3z9-ElFeA7WCTKSmI9aO4b_fakJWEz7tskp_KbiaVV3F0lZrmDH8FK5DOq78j156G5s1Cue4hRdp6qR_MFa5arGVqg=s0-d)
> Takribani Wafungwa 167 wameruhusiwa kupiga kura na hata wanahabari wameruhusiwa kuhojiana nao kupata maoni yao juu ya uchaguzi huu (picha inajieleza)
> Tume ya Uchaguzi(IEBC) imekanusha kukwama kwa zoezi la Uchaguzi huko Kisumu. Wamesema kila kituo kuna vifaa vya akiba
> Gavana Wycliffe Oparanya amepiga kura katika Shule ya Msingi ya Mabole, Butere. Amewataka Wakenya kufanya uamuzi wa busara
11:30am updates:
> Waziri wa Kilimo katika Kaunti ya Meru, Genaro Gatangugi na Mbae Kiugo wameshambuliwa na wananchi baada ya kufumaniwa wakinunua vitambulisho eneo la Imenti Kusini
12:00pm updates:
> Mgombea Urais, Raila Odinga(NASA) anaelekea kupiga Kura katika kituo cha shule ya msingi Kibera
> Mgombea Urais kwa tiketi ya Jubilee, Uhuru Kenyatta amepiga kura katika kituo cha Shule ya Msingi Mutomo, Gatundu Kusini
> Mwanamume mmoja mwenye umri wa miaka 64, Patrick Wame amezirai na kufariki dunia baada ya kupiga kura ktk kituo cha Lela, Nyando.
> Maafisa wawili wa Tume ya Uchaguzi(IEBC) wanashikiliwa na Jeshi la Polisi kwa tuhuma za kujaribu kubadili majina ya makarani wa vituo. Maafisa hao walitaka kuwaweka Makarani wanaowataka wao kinyume na utaratibu. Tukio limetokea Kandara, Murang'a.
> Watu 24 wamejeruhiwa katika kituo cha Shule ya Msingi Moi Avenue baada ya kukanyagana wakati wakisubiri kupiga kura.
======
3: 00 PM UPDATES
> Mwanamke mmoja amejifungua Mtoto wa Kike katika kituo cha kupigia kura kilichopo Pokot Kaskazini. Mtoto huyo amepewa jina la Chepkura kwasababu amezaliwa siku ya uchaguzi.
> Mawakala watatu wa Jubilee wanashikiliwa na Polisi kwa tuhuma za kuendesha zoezi la kuhesabu kura ktk Kituo cha Heshima Shule ya Msingi.
> Gari moja lenye namba za usajiri bandia za KBY 840C likiwa katika msafara unaolindwa limekamatwa na Maafisa wa Jeshi la Polisi na kukutwa na karatasi za kura ziliwe zimewekewa alama kwa Wagombea wa Jubilee. Limekamatwa huko traveling under escort found carrying (KIEMS) Mandera, Banissa.
>
Mwenyekiti wa Tume ya Uchaguzi(IEBC), Wafula Chebukati atoa taarifa fupi ya namna Uchaguzi unavyoendelea nchini humo.
=====
4: 00 PM UPDATES
> Rais mstaafu wa Kenya, Mwai Kibaki, amekwama kupiga kura baada ya kukosa jina lake kwenye orodha ya majina ya wapiga kura iliyotolewa na Tume
> Katika vituo vipatavyo 40,883 vya kupigia kura, vituo sita vilikuwa na mpiga kura mmoja aliyeandikishwa.
> Raia wa kenya 4,300 walijiandikisha katika nchi za Tanzania, Uganda, Rwanda, Burundi na Afrka Kusini. Wamepiga kura katika nchi hizo.
5:34 PM
> Hatimaye Rais Mstaafu, Mwai Kibaki afanikiwa kupiga kura ikiwa ni dakika 34 baada ya muda wa kupiga kura kuisha.
> Mwenyekiti wa Tume ya Uchaguzi(IEBC), Wafula Chekibukati amesema vituo 300 vimeongezewa muda wa kupiga kura kutokana na changamoto mbalimbali.
Ametoa mfano wa baadhi ya vituo hivyo na changamoto zilizojitokeza;
Viongozi wa NASA wayakataa matokeo yote yaliyokwishatangazwa na IEBC kwa madai kuna faulo zinachezwa kwani fomu nambari 34A haijatumika kama sheria inavyoelekeza.
======
9th August, 2017
UPDATES 12:00 PM
> Kiongozi muandamizi wa NASA, Kalonzo Musyoka amewataka Wakenya kuwa watulivu. Wanaendelea kufuatilia malalamiko ya udukuzi.
> Askari Polisi wamewatawanya kwa mabomu ya machozi wafuasi wa Raila Odinga waliokuwa wameanza kuandamana.

1: 30 PM
> Wanaharakati wameungana na Raila Odinga kuyakataa matokeo ya Uchaguzi. Wameituhumu IEBC kumpendelea Uhuru Kenyatta.
> Mtu mmoja amefariki kwa kupigwa risasi na Askari wa Jeshi la Polisi akiwa nje ya kituo cha kujumlishia kura cha Shule ya Sekondari ya Wasichana ya Nduru kilichopo Kusini mwa Jimbo la Mugirango.
> KENYA: Tume ya Uchaguzi(IEBC) imetangaza kuyafuta matokeo ya Uchaguzi ktk kituo cha Enenkeshui Jimbo la Kilgoris.
> MACHAKOS: Mgombea wa nafasi ya Ugavana, Bi. Wavinya Ndeti ameyakataa matokeo ya awali yanayoonesha mpianzani wake bwana Alfred Mutua anaongoza. Amelalamika na kudai ameibiwa kura.
> Makamu Mwenyeiti wa Tume ya Uchaguzi(IEBC), Consolata Nkatha ametangaza kuanza kwa zoezi la kuhesabu kura za Urais kupitia Fomu namba 34A.
> NAIROBI: Watu wawili wameuawa kwa kupigwa risasi baada ya waandamaji kuwashambulia Askari wa Jeshi la Polisi katika mitaa ya Mathare.
FUATILIA HAPA MATOKEO YA UCHAGUZI
RESULTS

- Wafula Chebukati akiongea na Waandishi wa habari asema zoezi la Uchaguzi linaendelea vyema kwa maeneo mengi nchini humo.
- Zoezi la kupiga kura linaendelea vyema Magerezani, kwa yale maeneo yaliyochelewa kuanza kupiga kura wataongezewa muda.
- Chebukati: Vituo vitatu vilivyopo Laikipia vilipata changamoto za kiusalama lakini changamoto hizo zimetatuliwa na zoezi la kupiga kura linaendelea.
=====
4: 00 PM UPDATES
> Rais mstaafu wa Kenya, Mwai Kibaki, amekwama kupiga kura baada ya kukosa jina lake kwenye orodha ya majina ya wapiga kura iliyotolewa na Tume
> Katika vituo vipatavyo 40,883 vya kupigia kura, vituo sita vilikuwa na mpiga kura mmoja aliyeandikishwa.
> Raia wa kenya 4,300 walijiandikisha katika nchi za Tanzania, Uganda, Rwanda, Burundi na Afrka Kusini. Wamepiga kura katika nchi hizo.
5:34 PM
> Hatimaye Rais Mstaafu, Mwai Kibaki afanikiwa kupiga kura ikiwa ni dakika 34 baada ya muda wa kupiga kura kuisha.
> Mwenyekiti wa Tume ya Uchaguzi(IEBC), Wafula Chekibukati amesema vituo 300 vimeongezewa muda wa kupiga kura kutokana na changamoto mbalimbali.
Ametoa mfano wa baadhi ya vituo hivyo na changamoto zilizojitokeza;
- Huko katika Kaunti ya Turkana vituo 18 havikufunguliwa kwa wakati kutokana na kunyesha kwa mvua kubwa kuanzia usiku wa kuamkia leo.
- Jimbo la Ndia ambalo linavituo vya kupigia kura vipatavyo 70 ambavyo vilikumbwa na changamoto ya kuishiwa na karatasi za kupigia kura. Pia Vituo vya Nakuru Mashariki(Eneo lenye vituo 185) vilikumbwa na changamoto hiyo.
Viongozi wa NASA wayakataa matokeo yote yaliyokwishatangazwa na IEBC kwa madai kuna faulo zinachezwa kwani fomu nambari 34A haijatumika kama sheria inavyoelekeza.
======
9th August, 2017
UPDATES 12:00 PM
> Kiongozi muandamizi wa NASA, Kalonzo Musyoka amewataka Wakenya kuwa watulivu. Wanaendelea kufuatilia malalamiko ya udukuzi.
> Askari Polisi wamewatawanya kwa mabomu ya machozi wafuasi wa Raila Odinga waliokuwa wameanza kuandamana.
> Wanaharakati wameungana na Raila Odinga kuyakataa matokeo ya Uchaguzi. Wameituhumu IEBC kumpendelea Uhuru Kenyatta.
- Wanaharakati wameungana na Raila Odinga kuyakataa matokeo ya Uchaguzi. Wameituhumu IEBC kumpendelea Uhuru Kenyatta.
- Chini ya Kempeni ya 'Kura Yangu Sauti Yangu' wamesema matokeo yamekiuka Katiba kwani hayajaambatanishwa na Fomu 34A.
- Kiongozi wa Wanaharakati hao, amedai Sheria inaitaka Tume ya Uchaguzi kutoa Fomu namba 34A lakini hawajafanya hivyo.
- Kundi hilo limeenda mbali na kudai Tume ya Uchaguzi(IEBC) imepunguza kura za Raila Odinga na kumuongezea Uhuru Kenyatta.
- Mfano matokeo ya Uchaguzi ktk vituo vya Dagoretti, Langata, Nandi, Kisumu na Kepchebor yametofautiana na nakala za Fomu.
> Mtu mmoja amefariki kwa kupigwa risasi na Askari wa Jeshi la Polisi akiwa nje ya kituo cha kujumlishia kura cha Shule ya Sekondari ya Wasichana ya Nduru kilichopo Kusini mwa Jimbo la Mugirango.
- Mmmoja wa mashuhuda bwana Evans Okemwa amesema Mwanaume huyo amepigwa risasi mgongoni huku akilalamika kuwa hakukuwa na sababu ya msingi ya Askari huyo kufanya unyama huo.
- Kamanda wa Polisi wa Kisii, Abdi Hassan amesema kuwa Askari huyo aliyefanya tukio hilo tayari amewekwa rumande kwa hatua zaidi za kisheria.
- Shuhuda mwingine Bi. Evelyn Nyaboke amesema alimuona marehemu akijaribu kuwaamua wenzie wawili waliokuwa wakipigana lakini chakushangaza ni kwamba Askari huyo ambaye alikuwa mbali na tukio hilo alifyatua bomu la machozi kisha kumpiga risasi kijana huyo.
> KENYA: Tume ya Uchaguzi(IEBC) imetangaza kuyafuta matokeo ya Uchaguzi ktk kituo cha Enenkeshui Jimbo la Kilgoris.
- Akitangaza hatua hiyo Afisa wa Tume ya Uchaguzi(IEBC), Elijah Ombogo amesema kuwa wamebaini idadi ya walioandikishwa ni 285 lakini kura zilizopigwa siku ya uchaguzi(Jana) ni 325.
- Ameahidi kumuunga mkono mgombea yeyote atayeibuka mshindi pia ameahidi kumpatia ushirikiano.
- Tutafanya mazungumzo na Wanasiasa, pia tutahusishwa katika kujumlisha kura mwisho tutatoa mtazamo wetu.
- Tunawaomba Wananchi wawe watulivu na sisi tutatoa mtazamo wetu utakao kuwa huru kabisa.
> MACHAKOS: Mgombea wa nafasi ya Ugavana, Bi. Wavinya Ndeti ameyakataa matokeo ya awali yanayoonesha mpianzani wake bwana Alfred Mutua anaongoza. Amelalamika na kudai ameibiwa kura.
> Makamu Mwenyeiti wa Tume ya Uchaguzi(IEBC), Consolata Nkatha ametangaza kuanza kwa zoezi la kuhesabu kura za Urais kupitia Fomu namba 34A.
> NAIROBI: Watu wawili wameuawa kwa kupigwa risasi baada ya waandamaji kuwashambulia Askari wa Jeshi la Polisi katika mitaa ya Mathare.
FUATILIA HAPA MATOKEO YA UCHAGUZI
RESULTS
Comments
Post a Comment