DAR: Mkuu wa Mkoa atengua agizo la Polisi kuhusu kutoa 'tinted'

Hadi polisi watakapotoa ufafanuzi zaidi kwa nini lifanyike!. Hapo awali Polisi Walipiga Marufuku Magari yenye vioo Vyeusi{Tinted}. zaidi soma=>UJAMBAZI: Magari yote yenye tinted yapigwa marufuku na Polisi jijini Dar

=========

Akizungunza kwa njia ya simu Mkuu wa Mkoa wa Dar amesitisha zoezi la kuondoa Tinted kwenye magari zoezi ambalo lingeanza kesho.

Hoja zake nimezipima zina mashiko mfano pale alipotetea tint kwamba ni mojawapo ya ulinzi wa vifaa na vitu ndani ya gari kupunguza ushawishi kwa watu kuviona na kuiba.

Akatolea mfano wanawake wanaoendesha magari halafu yuko peke yake kwenye gari uwezekano wa kufuatiliwa na majambazi ni mkubwa hivyo tint husaidia kupunguza watu wa nje ya gari kuona idadi ya watu waliomo kwenye gari.

Pia amesema magari ya mikoani yanatumika katika kusafiri kuja Dar sasa inabidi anapoingia Dar aidha apaki gari mpakani kuepuka kukamatwa na sakata la gari yake kuwa na tint au kutokutumia magari hayo kuja Dar kitu ambacho anasema si sahihi maana mtu kanunua gari limsaidie kusafiri.

Kifupi Mkuu wa Mkoa amesitisha zoezi hilo mpaka hapo jeshi la Polisi litakapompatia maelezo ya kutosha.

Pia amesisitiza bado jeshi la pollisi linao uwezo wa kudhibiti wahalifu wachache wanaotumia magari ya vioo vya tinted kufanya uhalifu.

Nawasilisha.
chanzo cha habari channel ten saa moja

Comments

Popular posts from this blog

Jinsi ya kutengeneza SABUNI ya kipande

Kumbukumbu ya kuundwa kwa chama cha AA mwaka 1927 chini ya Sesilia Matola