Baraza La Usalama La UN Launga Mkono Kuwekewa Vikwazo Kwa Korea Kaskazini


Baraza la usalama la Umoja wa mataifa, limeichukulia hatua Korea Kaskazini kwa hatua yake iliyochukua mwezi uliopita ya kuifanya majaribio ya zana zake za kitonoradi(makombora).
Baraza hilo lilipiga kura ya pamoja katika kuidhinisha vikwazo vipya, vinavyolenga biashara ya chuma na mkaa ya mawe ya Pyongyang, Pyongyang huuza bidhaa hizo nje kwa zaidi ya dola bilioni kwa mwaka.
Pia rais wa Marekani Donald Trump, alipongeza hatua za China na Urusi za kuunga mkono vikwazo hivyo vilivyotolewa na baraza hilo la Umoja wa mataifa. Anasema kuwa, vikwazo hivyo, vitakuwa na “athari kubwa mno” ya kibiashara.
Majirani wao Korea Kusini, wameiomba Korea Kaskazini kufuata njia ya mazungumzo, ili kutatua mzozo huo uliopo kwa Pyongyang, kuhusu zana za kinyuklia.
Si hao tu lakini hata Beijing pia inaomba kurejelewa kwa mazungumzo.

Comments

Popular posts from this blog

Jinsi ya kutengeneza SABUNI ya kipande

Kumbukumbu ya kuundwa kwa chama cha AA mwaka 1927 chini ya Sesilia Matola