UKWELI HUU HAPA kuhusu KIFO CHA IVAN mume wa ZALI
Kumbukumbu ya kuundwa kwa chama cha AA mwaka 1927 chini ya Sesilia Matola
Ilikuwa mwaka 1927 ndipo chama cha AA kiliundwa kwa msaada wa Gavana wa Kiingereza nchini Tanganyika Sir Roland Davidl Cameron na Dr Agrey raia wa Ghana mwenye mtaa Kariakoo ya leo, huyu Mghana alikuwa mshauri wa kisheria na kimuundo tu, kikawa kinafanyia shughuli zake nyumbani kwa Rais wa kwanza wa AA bwana Cecil Matola kutoka kabila la wayao, na miaka mitatu baadae, yaani 1930 ndipo wakapata jengo toka kwa Gavana Donald Cameron, hapo ndipo picha hii ilipigwa, Mwaka 1933 Cecil Matola alifariki dunia, na nafasi yake ikakaimiwa na katibu mkuu wa AA Bwana Kleist Sykies (ambae baba yake mzee Platanta alikuwa ni muhamiaji haramu toka Afrika Kusini aliyefika Tanga na kuanzisha makazi huko baada ya kuwa mateka wa wajerumani vita ya kwanza ya dunia), mpaka mwaka 1948 chama kilipobadilishwa jina nakuwa TAA chini ya Rais wake Daktari Vedasto Kyaruzi (Mhaya), Hapo Rais wake wa kwanza wa TAA akawa Daktari Vedasto Kyaruzi, na katibu akawa Abdulwahid Klest Sykies, miaka miwili baadae, Dr Kyaruzi ...
Comments
Post a Comment