Posts

Jinsi ya kutengeneza SABUNI ya kipande

Image
Utengenezaji wa sabuni hii una njia nyingi Hatua  ya kwanza Chemsha vipimo 7 vya mafuta ya mawese au mafuta ya shea hadi ifikie hatua ya kimiminika chuja na yaweke kwenye chungu cha mfinyanzi au chombo cha plastiki. Hatua ya pili Pima vipimo 5 vya maji baridi kwenye chombo cha plastiki ongeza kipimo 1cha sodium hydroxide kwa uangalifu mkubwa kwenye maji acha hadi mchanganyiko huo uyeyuke. Subiri mchanganyiko wa sodium hydroxide na mafuta ukaribie kupoa. Hatua ya tatu Taratibu ongeza mchanganyiko wa sodium hydroxide kwenye mawese,huku ukikoroga haraka haraka bila kusitisha ukitumia ubao .hii ni njia nzuri zaidi. Njia ya pili Chemsha mafuta kwenye joto la kadiri ya 55C Changanya maji na sodium hydroxide na uache mchanganyiko huu upoe hadi kufikia joto hilohilo. Baada ya kuandaa mchanyiko wako changanya vimiminika hivyo viwili huku ukikoroga kwanguvu sana kadiri uwezavyo, taratibu sabuni itageuka kuwa laini. Kabla sabuni haijawa ngumu mwaga sabuni ndani ya kasha la mbao lilotanguli...

Watumishi Benki wapigwe stop simu za mikononi

Image
MKURUGENZI Mtendaji wa Taasisi ya Mabenki Tanzania (TIOB), Patrick Mususa amesema matumizi ya simu binafsi za mkononi yanayofanywa na baadhi ya wafanyakazi wa mabenki wakati wa kazi, yanapaswa kudhibitiwa. Badala yake amesema, simu za mezani za ofisi zitumike wakati wote wa kazi wanapowahudumia wateja. Kutokana na baadhi ya wafanyakazi wa benki kuhusishwa na uhalifu wa kushambuliwa kwa risasi na kisha kuporwa fedha na majambazi kwa baadhi ya wateja wao, mkurugenzi huyo wa TIOB amesema matumizi ya simu binafsi kwa wafanyakazi wa benki yanatakiwa kufanyika nje ya eneo la benki baada ya kazi. “Zitumike simu za ofisi wakati wa kazi tena kwa matumizi ya kiofisi ikiwemo kuwahudumia wateja wao. Mteja anaweza kuruhusiwa kutumia simu yake ndani ya benki pale tu anapotakiwa kufanya muamala na benki husika,” alieleza Mususa alipozungumza na gazeti hili. Mususa alisema taasisi yake inahusika na kutoa masomo ya kitaaluma ya mwaka mmoja kwa wafanyakazi wa mabenki ili kuwajenga kitaaluma na kima...

TATA GESTI: Wasiojulikana waua wawili chumba kimoja

Image
UTATA umeibuka baada ya miili ya watu wawili waliouawa na watu wasiojulikana kukutwa katika nyumba ya kulala wageni mjini Tanga ikiwa haina nguo na imefungwa kamba za miguu na mikononi. Katika tukio hilo ambalo limethibitishwa na Kamanda wa Polisi Mkoa wa Tanga, Benedicto Wakulyamba miili ya watu wawili, wote wanaume, iligunduliwa jana majira ya saa mbili asubuhi na mhudumu wa nyumba ya kulala wageni ya Bomai Inn iliyopo Kata ya Majengo jijini hapa. Kamanda Wakulyamba aliwaambia waandishi wa habari jijini hapa jana kuwa mhudumu wa nyumba hiyo ambaye hakumtaja kwa jina, alibaini kuwapo kwa miili hiyo alipotaka kufanya usafi ndani ya chumba hicho. "Majira ya saa mbili asubuhi wakati mhudumu alipoingia ndani ya chumba hicho namba 303 kwa ajili ya kufanya usafi, alikutana na miili ya watu hao wawili wote ni wanaume ikiwa imelala chini, imefungwa kamba miguuni na mikononi," alisema. Kamanda huyo alisema miili hiyo ni ya watu wanaokadiriwa kuwa na umri wa kati ya miaka 35 na 4...

Tundu Lissu ametangazwa shujaa huko Lagos nchini Nigeria magharibi mwa bara la Afrika

Mbunge wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Tundu Lissu, ametangazwa katika kongamano la kimataifa lililofanyika jijini Lagos, nchini Nigeria, kuwa ndiye mwanasiasa kiongozi katika kutetea matumizi mazuri ya raslimali za taifa lake,anaandika Jabir Idrissa. Wanakongamano waliokusanyika kujadili amani duniani, wamesema: “Lissu ni kielelezo kizuri cha kiongozi mwenye maadili na shujaa wa haki za binadaamu… mpenda haki na mwanasiasa mkweli anayestahiki kuombewa na wapenda amani hata kufikia kuwa rais katika nchi yake.” Kwa ujasiri wake katika kukataa dhulma na kuitumia vema fani ya sheria katika kusimamia raslimali za taifa lake, wanakongamano wamesema, “mamilioni ya vijana duniani kote wameanza kuomba kusoma fani ya sheria vyuoni baada ya mitandao ya kijamii zaidi ya 11,000 kuripoti habari zake kwa muda wa siku 11 mfululizo kuliko habari za rais yoyote duniani.” Taarifa zilizofikia MwanahalisiOnline kutoka Nigeria, zimesema hatua hiyo imefikiwa kwenye kongamano lililomalizika jana likishi...

Yametimia ya Magufuli baki, Nkamia awasilisha mswada rais kukaa madarakani miaka 7 kama Kagame

Image

HAYA HAPA MAGAZETI YA LEO JUMAMOSI SEPTEMBA 16,2017 - NDANI NA NJE YA TANZANIA

Image